b

Ziggy Justine

Sunday, February 14, 2016

Historia ya Valentine

V.A.L.E.N.T.I.N.E

Historia ya sikukuu ya Valentine ni  ya kawaida sana kiasi ambacho ni kwa wale ambao akili zao zimetekwa ma adui ndio hawataki kuelewa ukweli na wanatamani kufuata udhalimu.

Nianze kwa kifupi kusema kuwa katika nyakati za utawala wa kirumi mwezi wa Februari ulikuwa ndio mwezi wa mwisho wa mwaKa (kama sasa tunavyosema, Desemba), na ulikuwa na siku 30.
Kaisari Juliasi akaamua kuita mwezi mmoja kwa jina lake – yaani Julai, na akaamua kuongeza  siku moja kwa mwezi huu na kuondoa kwenye Februari. Hivyo Februari ikawa na siku 29 tu. Baadae, Kaisari Oktavian ambaye aliitwa pia Kaisari Agusto alitawala. Naye pia akaita mwezi mmoja kwa jina lake – yaani Agosti, na kuuongeza siku moja akiitoa kwa Februari hii hii. Februari ikabakiwa na siku 28 tu

Sio hivyo tu, pia Waruni waliamini kuwa kila mwezi una pepo lake ambalo huanza kuwa na nguvu mwanzo wa mwezi, na kuwa na nguvu sana katikati ya mwezi, na nguvu kupungua hadi mwisho wa mwezi ambako kuachia pepo jingine la mwezi mwingine. Hivyo Warumi waliamini kuwa tarehe 15 ya kila mwezi ni tarehe ambayo pepo wana nguvu sana. Ndio siku wachawi, walogi na waganga hufanya uchawi wako.

Kwa sababu sasa Februari ilikuwa na siku 28, kati ya mwezi ilikuwa ni tarehe 14 ya Februari.  Iliitwa Kilele (Ides) ya mwezi. Sasa kwa kiwa “ides” ya mwezi huu  ni 14 Februari, basi usiku wa tarehe 13 ulikuwa wa muhimu sana kwa wachawi na pepo. Namba 13 ni ya kishetani, hivyo tarehe hii ya 13 kuamkia 14 ikawa ya muhimu sana kwenye uchawi wa kirumi na utawala wa kirumi.

Siku hii ya 14 Februari iliitwa LUPERCALIA au” Sikukuu ya Mbweha”. Ilikuwa ni siku ya kuzini zana kama vichaa bila kujizuia kwa ajili ya ibada ya mungu mke aitwaye JUNO. Siku hii pia ilikuwa ya kuabudu miungu ya kirumi iitwayo Lupercus na Faunus na siku ya kuwakumbuka mapacha wawili wanaodhaniwa kuwa ati waliishi duniani na kuwa ndio waanzilishi wa Urumi. Vijana hawa waliitwa Remus na Romulus, na warumi waliamini kuwa ati walipozaliwa walitupwa kwenye pango la kilima cha Palatine huko Urumi, na kunyonya maziwa ya mbwa mwitu wakaishi.

Pango hili liliitwa Lupercal, na na lilikuwa ndio kitovu cha sherehe za usiku wa Lupercalia au Februari 14.Kwenye siku hii ya Lupercalia – ambayo baadae iliitwa Siku ya Valentine, ma-Luperci – au makuhani wa Lupercus walivaa ngozi mbichi za mbuzi zenye damu – kwa ajili ya sherehe ya damu. Makuhani hawa walitoa kafara za mbuzi na mbwa na kuipaka miili yao damu wakawa wekundu. Damu waliyopaka ni ya kafara za mbuzi na mbwa. Sasa wale makuhani hutengeneza mikanda ya ngozi mbichi wa mbwa na mbuzi na kuzichovya kwenye damu. Hii mikanda iliitwa FEBRUA.

Wanawake wa kirumi walikaa kuzunguka kilima hili cha Palatine, na makuhani hawa hupita wakikimbiakimbia kipepo huku wameshikilia Februa. Hutumua mikanda hii kuwapiga wanawake hawa nao huchurwa alama za damu.

Baada ya ibada hii, wanawake vijana hukusanyika mjini na kuandika majina yao kwenye vikaratasi – nama kwenye kura, na kuweka kuwenye sanduku kubwa. Sanduku hili kuchanganywa kama kwa bahatunasibu. Vikaratasi hivi waliviita “Alama za upendo” – au “Love Note” – na waliziita “Billets”. Sasa wanaume wa Urumi hufika na kila mmoja kuchukua kikaratasi kimoja. Lile jina lililoandikwa kwenye kikaratasi ni la mwanamke ambaye mwanamume huyu atazini naye  na kuwakiana tamaa hadi sikukuu nyingine mwaka mwingine, tarehe 14 Februari.

Basi tangu kale, Februari 14 imekuwa siku ya zinaa sana na uchafu. Rangi nyekundu ilikuwa ni ya muhimu sana kwa sababu ni rangi ya damu ya kafara kwa miungu. Kile kitu ambacho watu sasa wanakiita moyo, sio moyo, wala maana yake tangu kale haikuwa kumaanisha moyo, kwa sababu hata moyo haufanani hivyo. Maana yake ni kielelezo cha umbile ka via vya mwanamke – na walisema kuwa hapo ndipo kwenye chemchem ya kuingilia  kwenye tendo la “zinaa takatifu”
Bwana akitupa neema tutaeleza kidogo neno hili Valentine lilitoka wapi. Kwa kifupi ni kuwa hakuna “mtakatifu Valentine”. Ni muhimu kujua kuwa Wavalentina ni wakatoliki wa kwanza waliokuwa kutawala Urumi karne ya 3







No comments:

Post a Comment