Histolia ya Krismasi
Wakati
wa zama za kale, siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za
Kusini kulisherehekewa mfano wa usiku ambao mungu wa Mama Watakatifu
alijifungua mtoto akijulikana kuwa ni mungu wa Jua. Pia (siku hii)
inaitwa Yule, siku ambayo inasherehekewa mno kwa kurushwa pashpashi.
Ambapo kila mtu atacheza na kuimba ili kuliamsha jua kutokana na
usingizi wake mnono wa majira ya baridi.
Wakati
wa Warumi, iliadhimishwa kwa kumsifu Satunusi (mungu wa mavuno) na
Mithrasi (mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia jua ambao
umekuja ukitokea Syria hadi Urumi. Karne kabla ya madhehebu ya Sol
Invictus, ilitangaza ya kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele, na
kwamba maisha yanasonga mbele, na ni mualiko wa kubaki kwenye nguvu
nzuri.
Siku
ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za mviringo za Kusini ni
baina ya siku ya 20 au 22 Disemba. Warumi waliadhimisha Saturnalia baina
ya tarehe 17 na 24 Disemba...
Wakristo wa kale
Ili
kuepuka kuchunguzwa wakati wa sherehe ambazo ni za wapagani, Wakristo
wa kale walikaa majumbani mwao pamoja na mtakatifu Saturnalia. Kwa vile
idadi ya Wakristo iliongezeka na mila zao zikaenea, sherehe zikachukua
shuruti za Kikristo. Lakini, Makanisa ya kale hakika hayakusherehekea
mwezi wa Disemba kwa kuzaliwa Kristo hadi alipokuja Telesforusi Telesphorus,
ambaye alikuwa askofu wa pili wa Roma kutoka mwaka 125 hadi 136 M,
askofu huyo ndiye aliyetangaza kwamba huduma za Kanisa zifanywe wakati
huu ili kuadhimisha “Kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mwokozi”. Hata hivyo,
kwa vile hakuna mtu hata mmoja aliye na uhakika wa mwezi ambao amezaliwa
Kristo, kawaida ya Uzawa ulikumbukwa Septemba, ambao ulikuwa ni wakati
wa Sherehe za Kiyahudi za Trumpetsi (kwa sasa ni Rosh Hashanah). Ukweli
ni kuwa, kwa zaidi ya miaka 300, watu walielewa kuzaliwa kwa Yesu katika
tarehe tofauti.
Katika
mwaka 274 M, kikomo cha jua kiliangukia tarehe 25 Disemba. Mfalme wa
Roma aitwaye Aurelian alitangaza tarehe hiyo kama ni “Natalis Solis
Invicti”, ‘Sherehe Ya Kuzaliwa Jua Lisiloshindikana’. Katika mwaka 320
M, Papa Julius I aliitangaza tarehe 25 Disemba kama ni tarehe rasmi ya
kuzaliwa Yesu Kristo.
Mnamo
mwaka 325 M, Krismasi ilitangazwa rasmi, lakini kiujumla haikutiliwa
maanani. Mtakatifu Constantine, ambaye ni Mfalme wa mwanzo wa dhehebu la
Ukristo la Kirumi, aliitanguliza Krismasi kama ni sherehe isiohamishika
kwa tarehe 25 Disemba. Pia aliitanguliza Jumapili kama ni siku kuu
ndani ya siku saba za wiki, na aliitanguliza (Pasaka) kama ni sherehe
yenye kuhamishika. Mnamo mwaka 354 M, Askofu Liberius wa Rumi, alitoa
amri rasmi kwa wafuasi wake kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu ndani ya
tarehe 25 Disemba.
Hata
hivyo, ingawa Constantine aliifanya rasmi tarehe 25 Disemba kama ni
sherehe ya kuzaliwa Kristo, Wakristo wakiitambua kama ni tarehe ya
sherehe iliyofanana na mapagani, hawakushiriki katika mambo mazuri (kwa
siku hii) iliyopangwa na Askofu. Krismasi ilishindwa kupata utambulisho wa kilimwengu miongoni mwa Wakristo hadi kipindi cha hivi karibuni. Huko Uingereza England,
Oliver Cromwell alizipiga marufuku sherehe za Krismasi baina ya miaka
1649 na 1660 kupitia kwa inayoitwa Sheria za Rangi Samawati Blue Laws, akiamini kwamba iwe ni siku ya kumuabudu mungu tu.
Hamu
ya kuifurahia sherehe ya Krismasi ilikirimiwa pale Waprotestanto
(Wakristo wasiokubali baadhi ya mafundisho ya Kanisa la Kirumi)
walipokimbia uchunguzi kwa kutorokea sehemu za makoloni yote duniani.
Hata hivyo, Krismasi bado haikuwa ni sikukuu halali hadi miaka ya 1800.
Na, weka akilini, hakukuwa na picha ya Baba Krismasi (Santa Claus) kwa wakati huo.
Krismasi inaanza kuwa maarufu
Umaarufu wa Krismasi ulianza ghafla mnamo mwaka 1820 kutokana na kitabu cha Washington Irving The Keeping of Christmas at Bracebridge Hall
‘Kuiadhimisha Krismasi Kwenye Jukwaa La Bracebridge’. Mnamo mwaka 1834,
Malkia wa Uingereza aitwaye Victoria, alimkaribisha mumewe wa
Kijerumani Prince Albert ndani ya Ngome ya Windso Windsor Castle, akimuonesha tamaduni za mti wa Krismasi Christmas tree na Nyimbo Za Kumsifu Yesu Kristo carols
ambazo ziliadhimishwa Uingereza kwa Mfalme wa Uingereza. Mwaka 1834,
wiki moja kabla ya Krismasi, Charles Dickens alichapisha Nyimbo za
Kumsifu Yesu za Krismasi Christmas Carols (ambapo aliandika kwamba Scrooge alimuamrisha Cratchit kufanya kazi, na kwamba Baraza Kuu la Marekani US Congress
lilikutana Siku ya Krismasi). Ilikuja kuwa ni maarufu mno hadi kufikia
kwamba sio makanisa wala serikali kukana umuhimu wa sherehe za Krismasi.
Mnamo mwaka 1836, Alabama ilikuja kuwa ni taifa la mwanzo ndani ya
Marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mnamo mwaka 1860,
mfananishi illustrator wa
Marekani aitwaye Thomas Nast alichukua kutoka hadithi za Kiingereza
kuhusu Mtakatifu Nicholas, muangalizi mtakatifu wa watoto, kumtengeneza
Baba Krismasi Father Christmas.
Mwaka 1907, Oklahoma ilikuwa ni ya mwisho miongoni mwa mataifa ya
Marekani kutangaza Krismasi kama ni sikukuu halali. Mwaka baada ya
mwaka, nchi za dunia nzima zilianza kuitambua Krismasi kama ni siku ya
kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu.
Nakuombea Krismasi Njema Have a merry Christmas
Leo,
mambo mengi yasiyokuwa ya Kikristo yananasibishwa ndani ya Krismasi.
Yesu alizaliwa mwezi wa Machi, bado siku yake ya kuzaliwa inasherehekewa
Disemba ya 25, wakati wa solstice.
Sherehe za Krismasi zinamalizikia siku kumi na mbili za Krismasi
(Disemba 25 hadi Januari 6), ni idadi hiyo hiyo ya siku ambazo
zilisherehekewa na wapagani wa ki-Rumi wakale kwa kuadhimisha kurudi kwa
jua. Hivyo, hakuna mshangano wowote kwamba Wakristo waliosafi puritans – au Wakristo wasiotaka mabadiliko conservative
– watahamaki kwa Krismasi kuwa “sio ya kidini kama ilivyotakikana
kuwa,” wakisahau kwamba Krismasi haikusherehekewa hata kidogo hadi siku
za hivi karibuni.
Yesu Alisemaje Kuhusu Krismasi?
Mazoea ya Krismasi
Mti
ulio bora wa Krismasi unanunuliwa. Ukipambwa kwa madoido yenye kung’ara
pamoja na kumetameta, unasimamishwa karibu na dirisha. Maduka
yanajazana wanunuzi wakisaka zawadi na vile viduchu vinasubiri kwa hamu
kubwa ya Baba Krismasi Santa.
Ni mshughuliko na ni homa ya Krismasi Christmas fever, umewahi kufikiri kabla? Je, Biblia au Yesu aliwahipo kusababisha homa ya Krismasi?
Tafakari juu ya mchanganuo ufuatao kuhusu Krismasi, na ukweli utakuja kuwa wazi zaidi na zaidi.
Je, Krismasi Ina Ushahidi wa Biblia?
Neno
‘Krismasi’ halipo ndani ya Biblia. Biblia ilifunga midomo ya sherehe
yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kitu kimoja; upambaji wa
mti. Biblia wenyewe inashutumu upambaji wa miti (ya Krismasi):
“Mila
za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji
anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu,
wanaugandanisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika” (Jeremia
10-3,4).
Wazungu
wa ki-Pagani kabla ya Ukristo, waliamini miujiza kwamba miti ya kijani
ina nguvu maalum za ulinzi. Hakika, matumizi ya Miti ya Krismasi imeanza
hivi karibuni tu mwa karne ya 17 huko Strasbourg,
Ufaransa na kutoka huko ukaenea hadi Ujerumani, Uingereza na baadaye
Marekani. “Ibada ya miti ilikuwa ni jambo la kawaida kwa dini miongoni
mwa watu wa Tyutoniki Teutonic na Skandinavia Scandinavia
wa Ulaya ya kaskazini kabla ya kuingia kwenye Ukristo…Walowezi wa
ki-Jerumani walileta mila za Mti wa Krismasi kwenye makoloni ya
Kimarekani mnamo karne ya 17. Kufikia karne ya 19, matumizi yake
yalienea sehemu tofauti”. (Angalia Encyclopedia ya Compton, Toleo la 1998)
Je, Yesu Alizaliwa Disemba ya 25?
Si
tarehe ya Disemba 25 wala tarehe nyengine yoyote iliyotajwa ndani ya
Biblia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Ilikuwa ni hivyo hadi kufikia mwaka 530
C.E kwamba mtawa monk
aitwaye Dionysus Exigus, aliweka tarehe isiyobadilika ya kuzaliwa kwa
Yesu kuwa ni Disemba 25. “Kulingana na taratibu za ki-Roma, alikosea
kuipanga tarehe ya kuzaliwa kwa Kristo (yaani, miaka 754 baada ya
kupatikana nchi ya Rumi) kama ni Disemba 25, mwaka 753”. (Angalia: Encyclopedia Britannica, toleo la mwaka 1998) Tarehe hii ilichaguliwa ili iendane pamoja na sikukuu ambazo zimeshagandana na imani za kipagani.
Mapagani wa Kirumi walisherehekea Disemba 25 kama ni ya kuzaliwa kwa ‘mungu’ wao wa nuru, aitwaye Mithra.
“Mnamo
karne ya pili M, hiyo sherehe ya Mithra ilikuwa ni ya kawaida zaidi
ndani ya Ufalme wa Rumi kuliko Ukristo, ambayo ilizaa mifanano iliyo
mingi” (The Concise Columbia Encyclopedia, toleo la mwaka 1995).
‘Waungu’
wengine wakipagani waliozaliwa Disemba ya 25 ni: Hercules mtoto wa Zeuz
(Wagiriki); Bacchus, ‘mungu’ wa mvinyo (Warumi); Adonis, ‘mungu’ wa
Kigiriki, na ‘mungu’ Freyr wa Ugiriki-mapagani wa Roma.
Je, Vipi Kuhusu Baba Krismasi Santa Claus?
Kama viumbe visivyokuwa binaadamu aliens
watafika duniani katika wakati wa Krismasi, bila ya shaka wataamini
Krismasi kuwa ni sherehe ya kufurahikia kuzaliwa kwa Baba Krismasi Santa. Majina ya ‘Santa Claus’, hayamo popote ndani ya Biblia.
Hata hivyo, Mtakatifu Nikolas Saint Nicholas (Baba Krismasi Santa Claus)
alikuwa ni mtu halisi, askofu, ambaye alizaliwa miaka 300 baada ya
Yesu. Kwa mujibu wa hekaya za kale, alikuwa ni mtu mwenye huruma mno na
alitenga nyakati za usiku kwenda kutoa zawadi kwa mafukara. Baada ya
kifo chake mnamo Disemba ya 6, watoto wa shule huko Ulaya walianza
kusherehekea siku hiyo kwa karamu kila mwaka.
Baadaye Malkia Victoria aliibadilisha sherehe hiyo kutoka Disemba ya 6 kuwa ni Disemba ya 24 kuamkia Krismasi.Imetafsiriwa Na: ‘Abdun-Naaswir Hikmany
Ime'Editiwa Na: Ziggy Justine Jr
No comments:
Post a Comment